Gesi bei chini, mkaa juu – Chalamila

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema ifike wakati bei ya gesi iwe chini na bei ya mkaa iwe juu. ili kuondokana na matumizi ya nishati chafu inayochangiwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Chalamila amesema hayo leo kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2024-2034 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (JNICC) Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi ni Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

“Mikoani wanasema sisi ndio tunashawishi sana kukata mkaa, na sisi tunaona wao ndio waliosababisha kukata miti kwa wingi,” amesema RC Chalamila.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/nishati-safi-ndio-mpango-mzima/

Hata hivyo amewataka wananchi wanaoishi vijijini kuhakikisha wana acha ukataji miti hovyo ili kusaidia kuruhusu kwa wingi matumizi sahihi ya Nishati ya Gesi.

Kaulimbiu katika hafla hiyo ni “Nishati Safi ya Kupikia kwa kila Mtanzania”

Habari Zifananazo

Back to top button