Gesi ya Mtwara kusambazwa Malawi

BALOZI wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole amesema mazungumzo kati ya Tanzania na Serikali ya Malawi ya Tanzania kuiuzia gesi asilia inayozalishwa mkoani Mtwara yamefikia hatua nzuri.

Balozi Humphrey Polepole amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari leo, kuwa “hatimaye mazungumzo ya miezi kadhaa yamezaa matunda” na kwamba “nimepata kibali cha kuanza kutekeleza mradi huu hapa Malawi.

Polepole amesema Serikali ya Tanzania iko tayari kuwezesha upatikanaji wa gesi asilia kutoka Mtwara na kupitia ushoroba wa Mtwara mpaka Salima, mkoa wa kati na pembezoni mwa Ziwa Nyasa ambapo kuna mradi unatekelezwa wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha megawati 75 na ghala la kuhifadhia gesi asilia.

Habari Zifananazo

Back to top button