GGR kuleta mabadiliko katika uongezaji thamani madini

GEITA: KIWANDA cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery (GGR) kinachomilikiwa na Mwekezaji Mtanzania Sarah Masasi kimeiweka Tanzania katika Soko la Kimataifa katika usafishaji wa dhahabu duniani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde leo Septemba 25, 2023 mkoani Geita baada ya kutembelea na kuzungumza na mwekezaji na wafanyakazi wa kiwanda cha kisasa cha kusafisha madini ya dhahabu cha GGR.
Mavunde amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kiwanda hicho kupata Ithibati
(ISO Certification) za aina tano ikilinganishwa na kiwanda kikubwa cha kusafisha madini ambacho hakina ISO zote hizo.
Aidha, Mavunde ameiagiza timu ya wataalam iliyoundwa ikihusisha wataalam kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Wizara ya Madini, wawakilishi wa wachimbaji wadogo na wamiliki wa viwanda vya usafishaji wa madini kuandaa taarifa itakayoelezea namna bora ya upatikanaji wa malighafi na ushiriki wa BoT kwenye kuwasaidia wachimbaji wadogo kuzalisha dhahabu itakayopelekwa kwenye viwanda hivyo.

Habari Zifananazo

Back to top button