Gharama uunganishaji umeme kutolewa baada ya utambuzi

SERIKALI inaendelea na utambuzi wa maeneo na wananchi wanaoishi kata za mjini zenye sura ya vijiji, ili iweze kupanga gharama mwafaka za kuunganisha umeme.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato baada ya Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula aliyetaka kujua lini serikali itaainisha bei rasmi za kuunganisha umeme maeneo ya kata za mjini zenye sura za vijiji.

Kuhusu muda, Naibu huyu amesema kuwa zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mnamo mwezi Desemba, 2022.

“Baada ya zoezi hili serikali itapanga bei mwafaka za kuunganisha umeme kulingana na uhalisia wa maeneo husika,” ameeleza.

Habari Zifananazo

Back to top button