Gharama wagonjwa wenye PF 3 zahojiwa bungeni

DODOMA; MBUNGE wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo, amehoji bungeni kwa nini watu waliopata ajali wakienda hospitali za Serikali na Fomu ya Polisi (PF3), hulipa gharama za kumuona daktari na kugonga muhuri.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel, amesema Serikali kupitia Sera ya Afya ya Mwaka 2007, imeweka utaratibu wagonjwa wote wa dharura kupatiwa huduma za afya za dharura kwanza pasipo kikwazo cha kulipia, hadi hapo changamoto za kiafya za dharura zitakapokwisha.

“Natoa wito kwa waganga wakuu wa vituo vyote kuhakikisha wagonjwa wa dharura wanapata huduma wanazostahili kwanza ili kuokoa Maisha yao, na taratibu nyingine zifuate baada ya kuwa wamehudumiwa, “amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

Back to top button