Gharama za upangaji, upimaji, umilikishaji ardhi zashuka

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ametangaza rasmi kushuka kwa gharama za upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi ambazo zimeridhiwa na Rais, Samia Suluhu Hassan.

Silaa ametangaza hayo kwenye uzinduzi wa kliniki ya ardhi katika Kata ya Chanika iliyopo halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi mbali mbali wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo la siku 25 lililoanza toka Desemba 16, 2023.

Amesema Rais ameridhia kushuka kwa gharama hizo ili kuwapunguzia mzigo wa gharama za upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi na kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi kwa urahisi.

Habari Zifananazo

13 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button