DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva Gift Stanford, ‘Gigy Money’ amesema kuwa wasanii wa bongo ni miyeyusho hawapendani wala hawasapotiani kwa jambo lolote.
Gigy amesema hayo jijini Dar es Salaam na kudai kuwa sio wasanii wote wanamoyo kama wake wa kusapoti na kuwapenda, wengi hawapendani.
“Mtu anaishi kama haitaji watu wengine kwenye maisha yao binafsi nawaitaji kiukweli tunategemeana ninachoona ni mtu hataki kuishi maisha yake, hataki kurudia nguo, rudia tu ndo maisha yetu ya kibongo,”amesema Gigy
Amesema, unakuta msanii anasema hana nguo ya kuvaa sio kweli vaa yoyote hata dera ni nguo ukitrendi umerudia nguo ila ni yako vaa tu binafsi ninawapenda na kusapoti ndo mana nina watu wanaonisapoti pia.