Giroud mfungaji bora Ufaransa

Mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud anakuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo, mara baada ya kufunga bao la kuongoza katika mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Poland hatua ya 16 bora mchezo ambao kwa sasa ni mapumziko.

Giroud sasa anafikisha mabao 52 akiwa na taifa hilo. Thiery Henry anashika nafasi ya pili akiwa na mabao 51 ambaye amestaafu kucheza soka na sasa ni kocha msaidizi wa kikosi cha Ubelgiji.

Antonio Griezmann ana mabao 42 na Michelle Platin ana mabao 41. Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ana mabao 37.

Habari Zifananazo

Back to top button