KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola anasema Jack Grealish atarejea kwenye kikosi kiwango chake kitakapoimarika.
Kiungo huyo wa Uingereza alikuwa katika kampeni ya kushinda ‘Treble’ msimu uliopita, ikijumuisha fainali za Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa.
Ameanza mechi 19 pekee msimu huu, zikiwemo saba za Ligi Kuu.
“Mchezaji yule yule, ana meneja yule yule, na jinsi tunavyocheza hajabadilika.
” alisema Guardiola.