Guardiola ampigia debe Potter

Mkufunzi wa Manchester City, Pep Guardiola amemtaka mmiliki wa Chelsea kuwa na subira dhidi ya kocha Graham Potter ambaye anapitia kipindi kigumu baada ya kupoteza michezo sita katika tisa ya mwisho.

Guardiola amezungumza kauli hiyo baada ya kuilaza The Blues mabao 4-0 katika mchezo wa Kombe la FA raundi ya tatu uliopigwa jana Uwanja wa Etihad.

“Nimwambie Todd Boehly ampe muda. Najua katika vilabu vikubwa matokeo ni muhimu lakini ampe muda. Alichokifanya Brighton ni bora. Wasimamizi wote wanahitaji muda.” alishauri Guardiola.

“Nikiwa Barcelona, nilikuwa na Lionel Messi ndio maana sikuhitaji misimu miwili lakini kila mtu anaihitaji muda.” alisema Guardiola.

Habari Zifananazo

Back to top button