Guardiola: Haaland anastahili heshima

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema mshambuliaji wa klabu hiyo, Erling Haaland anastahili heshima baada ya kufunja rekodi ya mabao EPL.

Bao moja alilofunga jana katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham, limemfanya Mnorwei huyo kufikisha mabao 35 kwa msimu mmoja na kuvunja rekodi ya Andy Cole na Alan Shearer wenye mabao 34.

Cole aliweka rekodi hiyo msimu wa 1993/1994 akiwa United, na Shearer kuweka rekodi hiyo mwaka 1994/1995 akiwa Blackburn Rovers.

“Kunapokuwa na hafla maalum, lazima tuonyeshe jinsi ilivyo maalum,” Guardiola alisema jana usiku, ambapo mara baada ya mchezo huo, benchi la ufundi la City lilitoa heshima kwa mshambuliaji huyo.

Haaland sasa amefikisha mabao 51 katika michuano yote msimu huu.

Habari Zifananazo

Back to top button