Guardiola tabu imeanza City
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kikosi chake kiko matatani kutokana na orodha ya majeruhi inayoongezeka.
–
Mhispania huyo amesema hali hiyo inatishia kuvuruga mipango na mwenendo mzuri wa klabu hiyo msimu huu.
–
Hatua hiyo imekuja baada ya Jana kiungo Bernardo Silva kufanyiwa mabadiliko baada ya kuumia. Guardiola amesema huenda Mreno huyo akakaa nje kwa wiki kadhaa.
–
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno anaungana na Kevin de Bruyne, Jack Grealish, Mateo Kovacic na John Stones ambao pia ni majeruhi.