Gundogan kuongoza 4-3-3 ya Xavi

BARCELONA imekamilisha usajili wa kiungo Ilkay Gundogan kutoka Manchester City.

Kwa mujibu wa wachambuzi mbalimbali kuhusu usajili huo, Gundogan ana uwezo wa kucheza namba 8 kwenye viungo wawili, lakini pia nyuma ya namba 9, mshambuliaji wa pili, amesaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.

Kwenye mfumo wa 4-3-3 wa Barcelona, huenda Xavi akamtumia Gundogan kwenye ‘partnership’ na Frank De Jong upande wa kushoto Franck Kessié baada ya kuondoka Sergio Busquets.

Pia wachambuzi wanaeleza kama ataamua kwenda na 4-2-3-1, De Jong kwenye viungo wawili na Kessie kisha Gundogan juu nyuma ya Lewandowski.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola timu ikiwa na mpira muundo wao unabadilika kutoka 3-2-4-1 kwenda 3-2-2-3, kwenye kiungo alikuwa akimtumia Gundogan kwenye namba 10 wawili na Kevin De Bryune kwenye wachezaji wawili wa mbele, pembeni Grealish, kati Haaland pembeni Bernado Silva au Mahrez.

Habari Zifananazo

Back to top button