KATIBU Mkuu Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameonya juu ya uwezekano wa vita kati ya Urusi na Ukraine kuwa inaweza kuenea zaidi na kuchochea upotevu wa amani duniani.
Akizungumza wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Jana Februari 6, 2023, Guterres amesema vita hivyo vimesababisha mateso makubwa kwa watu wa Ukraine huku vikiambatana na athari kubwa kwa dunia nzima.
Amesema dunia inaelekea katika vita vipana bila kujitambua, huku umwagaji wa damu ukizidi kuongezeka.
Amekemea vitisho vya kutumia silaha za maangamizi, akisema kinachozungumzwa na Urusi kuhusu matumizi ya nyuklia ya kimkakati hakiingii akilini.