Gwajima avalia njuga ubakaji ufukweni

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima amesema kuna haja ya kuweka mfumo maalumu katika fukwe ili huduma zinazotolewa kutambulika na watu wanaotoa huduma pia kutambulika lengo ni kuepuka watu matapeli ambao wanafanya ukatili.

Dk Gwajima ameeleza hayo katika ziara yake mwishoni mwa Juma katika fukwe za Coco na Kawe ili kujadiliana na watoa huduma za kuogelea (Beach boy) ikiwa ni hatua za kukomesha vitendo vya ubakaji kwa wasichana, vinavyofanywa na watu wachache wasiowaaminifu.

“Nilichoona hapa ni kuwa hawa vijana wanahitaji kuweka mifumo maalum ya watu kujua huduma wanazotoa na nimewaagiza watoe matangazo na vipeperushi vya huduma ili wanaokuja hapa wasikutane na matapeli kwani hii inachafua taswira yenu,”ameeleza.

Hivi karibuni kumekuwa na mijadala katika mitandao ya kijamii juu ya ukatilia wa ukabakaji unaofanywa na beach boy kwa wasichana wanaowafundisha kuogelea.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button