Gwiji wa Kiswahili, Ushairi afariki dunia

DAR ES SALAAM: BARAZA la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limetangaza kifo cha gwiji wa Lugha ya Kiswahili na ushairi nchini, Amiri Sudi Andanenga maarufu ‘Sauti ya Kiza’ kilichotokea usiku wa kuamkia Mei Mosi, 2024.

Kupitia taarifa ya BAKITA iliyotolewa leo imeeleza kuwa, Andanenga (88) amefariki dunia katika Hospitali ya Daktari Mvungi iliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“BAKITA linatoa pole kwa familia, wadau na wapenzi wa lugha ya Kiswahili pamoja

na Watanzania wote,” BAKITA imeomboleza.

https://www.instagram.com/p/C6a5EJwOmWO/

BAKITA imeeleza kumkumbuka Amiri Andanenga, Mzaliwa wa Kusini mwa Tanzania mwaka 1936 kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Lugha ya Kiswahili na fani yake ya Ushairi.

“Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi.

Amina…!!!,” imeeleza taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button