Haaland huyu ni tatizo EPL

BAADA ya kuweka kambani mabao mawili leo katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Man United, mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland sasa amefunga mabao 47 katika michezo 45 ya Ligi Kuu England.

Msimu uliopita Haaland aliibuka mfungaji bora wa ligi hiyo kwa kufunga mabao 36.

Msimu huu, mpaka sasa nyota huyo ameshafunga mabao 11 na ndiye anayoongoza orodha ya wafungaji bora.

Advertisement

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *