Haaland kuikosa Hispania

MSHAMBULIAJI wa Norway na klabu ya Manchester City, Erling Haaland atakosa mchezo dhidi ya Hispania na Georgia kufuzu mashindano ya Euro kutokana na majeraha ya nyama za paja. Shirikisho la soka nchini Norway (NFF) limethibitisha.

Katika taarifa yao NFF imeeleza kuwa badaa ya mchezaji huyo kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Burnley wiki iliyopita, alienda kujiunga na timu yake ya taifa na baada ya vipimo madaktari walithibitisha kuwa hatoweza kucheza michezo hiyo.

“Tulitumai kuwa angekuwa sawa, lakini baada ya kufanya majaribio jana ilibainika kuwa hatafanikiwa kwenye mechi dhidi ya Uhispania na Georgia. Ni bora apate mwendelezo wa matibabu katika klabu yake”. amesema daktari wa timu ya taifa Ola Sand.

Meneja wa timu ya Norway Ståle Solbakkenamesema wanafahamu ubora na umuhimu wa Haaland, lakini wamejipanga kuikabili Hispania bila mchezaji huyo na kwamba ubora na kwa nafasi yao watafanya vizuri katika mchezo huo utakaopigwa Machi 25, 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button