MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Erling Haaland atakuwa nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa mwezi Januari, kocha Pep Guardiola anasema.
Jeraha la mguu limemuweka nje Haaland tangu City ilipopokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Aston Villa mwezi Desemba.
Ilitarajiwa mfungaji bora huyo wa City angerejea kwa ajili ya Kombe la Dunia ngazi ya Klabu mwezi Desemba lakini jeraha bado halijapona.
“Ni mfupa. Inahitaji muda,” Guardiola alisema.