loader
Dstv Habarileo  Mobile
Messi alia kukosa penalti

Messi alia kukosa penalti

NYOTA wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi anasema kuwa ‘inauma’ baada ya penalti yake kuokolewa wakati timu yake ikitoka sare na Iceland katika mchezo wa Kombe la Dunia.

Nyota huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 30 alipiga penalti hiyo katika kipindi cha pili, lakini iliokolewa kirahisi na kipa upande wa pili, Hannes Halldorsson wakati matokeo yakiwa 1-1. Messi alikuwa akiangalia kumfikia mpinzani wake wa siku nyingi Cristiano Ronaldo, ambaye alianza vizuri fainali hizo za Kombe la Dunia kwa kufunga ‘hat-trick’ walipocheza dhidi ya Hispania Ijumaa usiku.

“Sasa inabadili mwongozo. Ilikuwa faida kwetu kupata penalti ile,” alisema. “Ni wazi inaniumiza mimi sana kukosa penalti ile. Walifungua kiasi na sisi tulipata nafasi zaidi. “Tumeumia sana kwa kutoondoka na pointi zote tatu, ambazo tulistahili kuzipata. Kwa kweli kuanza kwa ushindi siku zote ni jambo zuri, sasa inatubidi kufikiria mchezo wetu ujao dhidi ya Croatia.

“Tutajaribu kupata ushindi mapema. Messi alisema kuwa mbinu za Iceland ziliwafanya kuwa katika wakati mgumu na kuifanya timu yao kushindwa kupata ushindi kwani waliwazuia kucheza, lakini alikiri kikosi cha Heimir Hallgrimsson “kilicheza vizuri”. Nahodha huyo wa Argentina hadi sasa amekosa penalti nne kati ya saba zilizopita, ambazo alipiga kwa klabu yake na timu ya taifa. Kocha wa Argentina, Jorge Sampaoli alikataa kumlaumu mchezaji huyo na alimpongeza kwa tabia yake katika mchezo mgumu.

“Kuielezea na kuichambua kazi ya Lionel Messi ni ngumu kwa sababu haikuwa mechi nzuri kwake,”alisema. “Iceland walicheza mchezo wa kujilinda zaidi, wakizuia nafasi zote lakini tulifanya kila liwezalo ili kushinda, lakini tulishindwa licha ya Messi kujituma sana. “Wakati wote lengo letu ni kushinda na ndio maana sare imetuchangana sana.”

Kipa wa Iceland, Hannes Halldorsson alibainisha kuwa urefu ulimsaidia kuzuia shuti la Mess. “Nimeangalia penalti nyingi za Messi na zile ambazo nimekabiliana nazo na nikaona jinsi wanavyopiga na nikaona nifanye nini. “Ndoto yangu imekamilika kuokoa penalti, hasa iliyotusaidia tena kupata pointi, ambayo ni muhimu kwetu wakati tukijaribu kufuzu kwa hatua ya mtoano.” Halldorsson alikuwa shujaa juzi baada ya kuokoa penalti hiyo ya nyota Messi katika dakika ya 63 ya mchezo huo. Iceland, mchezo unaofuata itacheza dhidi ya Nigeria Ijumaa huko Volgograd.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8dfe9b89c051d62dfaa95e966fb6dbf2.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi