loader
Dstv Habarileo  Mobile
Salah hayuko fiti 100%

Salah hayuko fiti 100%

NYOTA wa Misri, Mohamed Salah juzi alihitaji msaada kutoka kwa wachezaji wenzake wawili ili kuvua jezi kutoka katika bega aliloumia, kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la AFP aliyekuwepo katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo.

Matumaini makubwa ya mafarao ni kutinga kwa mara ya kwanza katika hatua ya 16 katika Kombe la Dunia tangu mwaka 1990, timu hiyo imepiga kambi Chechen, ambao ni mji mkuu wa Grozny. Salah alikuwa akishuhudia kutoka katika benchi wakati Misri ikilala kwa bao 1-0, lililofungwa katika dakika ya 89 kwa kichwa na beki Jose Gimenez wakati wakifungwa na Uruguay Ijumaa.

Jumamosi mchezaji huyo alirejea katika mazoezi ya timu yake lakini alionekana akihitaji msaada kutoka kwa wachezaji wenzake watatu wakisaidia kumvua jezi. Dakatri wa timu hiyo hakuwa tayari kuthibitisha kuwa nyota huyo wa Liverpool yuko fiti kwa asilimia 100 na yuko tayari kucheza mchezo wa pili wa Misri dhidi ya wenyeji Urusi utakaofanyika Saint Petersburg Jumanne.

Lakini Salah angalau alikuwa na furaha wakati akikata keki ya siku ya kuzaliwa yenye kilo 100 katika sherehe ya kutimiza miaka 26 Ijumaa. Video iliyotolewa na mamlaka ya Chechen ilimuonesha Salah akitembea katika eneo la hoteli hiyo huku akisikiliza muziki. Alianza kutabasamu na kuhisi kuna kitu kisicho cha kawaida pale alipoona mfanyakazi wa hoteli hiyo akimpiga picha.

Baadae Salah alibaini keki kubwa katika meza. Juu imewekwa mfano wa kiatu cha rangi ya dhahabu, yenye umbo la taulo, ikiwa pamoja na mishumaa, ambayo ni zaidi ya 26. Mfanyakazi huyo wa hoteli haraka haraka alimkimbilia Salah akiwa na maikrofoni akimtaka atoe hotuba. Salah alionekana mwenye aibu, huku akionekana mwenye tabasamu wakati keki hiyo ikikatwa vipande vipande.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/db1a6fe68f4716976b2cc90cb9abbc92.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi