loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kombe la Dunia Urusi: Mechi 12, penalti saba!

Kombe la Dunia Urusi: Mechi 12, penalti saba!

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa leo alasiri (Jumatatu), Andars Granqvist amefanikiwa kufunga goli kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 65 ya mchezo na kuiwezesha Sweden kuilaza Korea Kusini 1-0.

Mechi hiyo ilikuwa ya 12 tangu fainali za Kombe la Dunia ziliponza mwishoni mwa wiki iliyopita huko Urusi.

Goli hilo limeifanya HabariLeo na SpotiLeo kupitia mechi zote zilizochezwa hadi sasa ambazo waamuzi wamekwisha hukumu ya penalti baada ya kujiridhisha kuwa madhambi yametendeka.

Kati ya mechi 12 zilizochezwa hadi leo, Jumatatu (haijumuishi mechi za Panama vs Ubelgiji na England vs Tunisia), waamuzi wametoa jumla ya penalti saba.

Kati ya penalti saba ndani ya mechi 12 zilizochezwa, wachezaji wameweza kufunga tano huku mbili zikishindwa kutinga kimiani, ikiwemo ile ya nyota Lionel Messi. Je, mashabiki wategemee penalti nyingi huko Urusi?

Endelea kufuatilia tovuti zetu kupata uhondo wa Kombe la Dunia huko Urusi.

Penalti zilizotolewa nchini Urusi na wafungaji Cristiano Ronaldo(Portugal vs Spain (alifunga)

• Antoine Griezmann (France vs Australia (alifunga)

• Miles Jedinak (Australia vs France (alifunga)

• Lionel Messi (Argentina vs Iceland (alikosa)

• Christian Cueva (Peru vs Denmark (alikosa)

• Luka Modric (Croatia vs Nigeria (alifunga)

• Andras Granqvist (Sweden vs South Korea (alifunga)

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/abfc64b4b7c344491ae00199a71a777a.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: Sauli Giliard

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi