loader
Dstv Habarileo  Mobile
Lukaku apiga 2,  Ubelgiji ikiua 3-0

Lukaku apiga 2, Ubelgiji ikiua 3-0

Mabao mawili yaliyofungwa na Romelu Lukaku na moja la Dries Martens yameipa Ubelgiji ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Panama katika mchezo wa Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea huko Urusi.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, hakuna iliyokuwa imeona lango za mwenzake baada ya kosa kosa za hapa na pale katika kipindi cha kwanza. Ubelgiji inayopigiwa upatu kuwa itafika mbali kwenye fainali hizo kutokana na ubora wa kikosi chake, ilipata goli la uongozi kupitia shuti kali la Martens katika dakika ya 47.

Lukaku, anayeichezea Manchester United, aliongeza mabao mawili katika dakika za 69 na 75 na kuihakikishia Ubelgiji ushindi na kutwaa pointi zote tatu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/24e9c7a989670724658a66eca4a260ac.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi