loader
Dstv Habarileo  Mobile
Senegal kuisafisha Afrika raundi ya kwanza Kombe la Dunia leo?

Senegal kuisafisha Afrika raundi ya kwanza Kombe la Dunia leo?

Mzunguko wa kwanza wa mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea huko Urusi unakamilika leo huku wawakilishi wanne kutoka Bara la Afrika wakiwa wamepoteza mechi walizocheza.

Wawakilishi ambao hawajacheza hata mechi moja, Senegal watajitupa uwanjani leo kukamilisha mzunguko wa kwanza kwa kuikabili Poland.

Matumaini ya Waafrika kuonja ladha ya ushindi katika mzunguko huo yanashikiliwa na 'Simba wa Teranga' ambao watamtegemea zaidi Sadio Mane katika safu ya ushambuliaji.

Huku Senegal ikijitupa uwanjani kukamilisha raundi hiyo, Mafarao wa Misri watajitupa uwanjani leo kuanza raundi ya pili dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo, Urusi. Timu nne za Afrika zilizopoteza mechi katika raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia ni:-

Croatia 2-0 Nigeria

Misri 0-1 Uruguay

Morocco 0-1 Iran

Tunisia 1-2 England

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/11ebbe12fa7055fbb328b11ccccbaa58.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: Sauli Giliard

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi