loader
Dstv Habarileo  Mobile
Maradona amuwakia kocha wa Argentina

Maradona amuwakia kocha wa Argentina

GWIJI wa soka Argentina, Diego Maradona alimlaumu na kumuonya kocha wa timu hiyo Jorge Sampaoli kwa kutoka sare dhidi ya Iceland katika mchezo wa Kombe la Dunia.

Alisema kuwa kama timu hiyo itaendelea kucheza hivyo, basi kocha huyo aisrudi Agentina. Lionel Messi alikosa penalti wakati timu hiyo ikijikuta ikilazimishwa sare na Iceland katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi D Jumamosi. Maradona, ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya taifa, alishuhudia mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Spartak.

Maradon alionesha kuchukizwa na sare hiyo, ambapo alisisitiza kuwa timu hiyo inatakiwa kugangamala ili kupata matokeo katika mechi zilizobaki ili ifuzu kwa hatua ya mtoano ya 16 bora. Katika mchezo huo, Argentina ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mkali wake mwingine, Sergio Aguero katika dakika ya 19 lakini Iceland, ikicheza kwa mara ya kwanza kabisa katika Kombela Dunia, ilisawazisha baadae kupitia kwa Alfred Finnbogason.

Messi alikuwa akiangalia uwezekano wa kutaka kumfikia mpinzani wake Cristiano Ronaldo aliyofanya katika Kombe la Dunia, baada ya Mreno huyo kufunga hat-trick walipocheza dhidi ya Hispania Ijumaa. Lakini penalti yake ya dakika ya 63 iliokolewa na kipa Hannes Halldorsson na alijaribu kuipenya beki iliyojipanga vizuri ya Iceland. “Siwalaumu wachezaji. Naweza kulaumu kazi iliyofanywa…,” alisema Maradona.

“Nilikosa penalti tano na bado nilibaki kuwa Diego Armando Maradona. Sifikiri kama walikosa pointi mbili kwa sababu Messi alikosa penalti,” aliongeza mchezaji huyo wazamani mwenye umri wa miaka 57, aliyeiongoza Argentina katika fainali za Afrika Kusini mwaka 2010. Argentina ilicheza na Croatia katika mchezo ujao huko Saint Petersburg Juni 21.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3a51fa204aa10a419626893582014b21.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi