loader
Dstv Habarileo  Mobile
Morocco kuibeba Afrika?

Morocco kuibeba Afrika?

MOROCCO leo wanatarajia kujaribu kuondoa jinamizi la kuanza michuano ya Kombe la Dunia vibaya itakapomenyana na mabingwa wa Ulaya, Ureno. Simba hao wa milima ya Atlas walianza vibaya michuano ya mwaka huu baada ya kujifunga bao la dakika za mwisho kupitia kwa Aziz Bouhaddouz katika mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Iran kwenye uwanja wa Saint Petersburg Ijumaa iliyopita na kuwafanya kuchapwa bao 1-0.

Wawakilishi hao wa Afrika wanakutana na Ureno ambao mechi ya kwanza walitoka sare ya mabao 3-3 na mabingwa wa dunia mwaka 2010, Hispania, huku nyota wake Cristiano Ronaldo akifunga mabao yote matatu hali inayofanya mabeki wa Morocco kuwa makini zaidi na mchezaji huyo wa Real Madrid.

Morocco haichukuliwi kama timu dhaifu, hasa kutokana na kufuzu kwake michuano hiyo ikiwa haijapoteza mechi hata moja kwenye kundi lake, hivyo hakuna shaka mechi ya leo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mechi hiyo ya kundi B inatarajiwa kuchezwa kuanzia saa tisa alasiri huku timu nyingine za kundi hilo, Iran na Hispania zikitarajiwa kujitupa uwanjani saa tatu usiku.

Hispania inahitaji ushindi baada ya kutoka sare mechi ya kwanza na Ureno. Kikosi cha Iran si cha kudharau, kina vijana wengi na wanaocheza soka safi. Kikosi kilichokwenda Brazil mwaka 2014 ndicho kilichokuwa na wachezaji wakongwe lakini msimu huu ni wachezaji watatu tu kwenye kikosi kile ndio walioanza katika mechi ya ufunguzi Urusi. Mechi nyingine itakayochezwa leo ni kati ya Uruguay na Saudi Arabia katika kundi A. Katika mechi ya mapema jana, Colombia iliangukia pua baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Japan.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6f3d5eb981df9340862b6d6de33bdbff.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi