loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ronaldo aing’oa Morocco

Ronaldo aing’oa Morocco

CRISTIANO Ronaldo ameendelea kung’ara kwenye michuano ya Kombe la Dunia Urusi baada ya jana kufunga bao la ushindi kwa timu yake ya Ureno lililoitupa nje ya michuano Morocco.

Macho yote yalikuwa kwenye uwanja wa Luzhniki ambapo nyota huyo wa Real Madrid alifunga mabao matatu katika mechi ya ufunguzi ya Ureno ikitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya mabingwa wa mwaka 2010, Hispania. Ilimchukua nahodha huyo dakika nne tu kuimaliza Morocco akiuwahi kwa kichwa mpira wa krosi wa Joao Moutinho na kuujaza wavuni. Bao hilo la Ronaldo linawaweka mabingwa hao wa Ulaya kileleni mwa kundi B kabla ya Hispania kucheza na Iran jana.

Lakini pia bao hilo linamfanya Mreno huyo kuongoza kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu. Morocco, ambayo wiki iliyopita ilikosa nafasi ya kuwania kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 imeungana na waafrika wengine Misri, kuaga michuano hiyo na sasa zinasubiri mechi za kukamilisha ratiba.

Ikishangiliwa na maelfu ya mashabiki wake, Morocco ilijitutumua na kupambana katka mechi hiyo lakini mipango yake ya hovyo kwenye umaliziaji iliimaliza. Mashuti yake mengi yaligonga mwamba na mara moja miamba hiyo ya Afrika ya Kaskazini ililenga shuti golini lakini kipa mpya wa Wolves, Rui Patricio alifanya kazi yake vizuri. Morocco ilifungwa na Iran bao 1-0 katika mechi yake ya kwanza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8a4ecbeba69cd387c149dfb51e9d288d.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi