loader
Dstv Habarileo  Mobile
Brazil yafufuka, yaichapa Costa Rica 2-0

Brazil yafufuka, yaichapa Costa Rica 2-0

Mabao mawili yaliyofungwa na Philippe Countinho na Neymar Jr katika muda wa majeruhi yameipa Brazil ushindi wa 2-0 dhidi ya Costa Rica.

Countinho amefunga goli lake la pili katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi katika dakika ya ya kwanza ya nyongeza huku mwamuzi akikaribia kupuliza kipenga chake kuashiria kumalizika kwa mechi hiyo,

Neymar aliihakikishia Brazil ushindi kwa kupachika bao katika dakika ya saba ya nyongeza. Hata hivyo, hilo linakuwa goli lake la kwanza tangu mashindano hayo yaanze nchini Urusi.

Baada ya mechi hiyo, Neymar alibaki uwanjani pekee yake akiwa amejifunika uso kwa viganja vyake huku akilia kwa muda kabla ya kuelekea kwenye vyumba vya wachezaji vya kubadilisha nguo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c676d43e3e4801bc7e9db55d5dc875ae.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: Na Janeth Mesomapya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi