loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nigeria yawacharaza 'wasumbufu' wa Argentina

Nigeria yawacharaza 'wasumbufu' wa Argentina

Nigeria imeamka na kuicharaza Iceland mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi D la Kombe la Dunia linaolendelea nchini Urusi. Ahmed Mussa aliwatoa kimasomaso Wanaigeria na Bara la Afrika kwa ujumla kwa kufunga mabao ya kiwango katika dakika za 49 na 75.

Hata hivyo, Iceland, taifa lenye idadi ndogo zaidi duniani, ilijitutumua baada ya kuruhusu magoli hayo mawili na kufanikiwa kupata mkwaju wa penalty, ambayo imepaishwa na Gylfi Sigurdsson katika dakika ya 83 ya mchezo.

Ikumbukwe kuwa Iceland iliushangaza ulimwengu baada ya kutoka sare ya 1-1 na vigogo Argentina hivyo, ilitarajiwa kuwa Nigeria ingepata upinzani mkubwa zaidi.

Baada ya kuonja ushindi huo, Nigeria imepanda hadi nafasi ya pili, nyuma ya vinara wa kundi E ambao ni Croatia yenye pointi sita. Iceland ipo katika nafasi ya tatu huku Argentina ikiburuza mkia kwa kujikusanyia na ponti moja tu hadi sasa.

Hatima ya Nigeria kusonga mbele ipo mikononi mwa Argentina kwani itahitaji sare yoyote ili ijihakikishie nafasi ya pili. Ushindi utaiweka katika nafasi nzuri zaidi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f416a8820c10e247eb0052095dd19ac6.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: Sauli Giliard

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi