loader
Picha

RC aagiza wakurugenzi watafute wawekezaji

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za Hanang, Mbulu, Kiteto, Babati na Simanjiro mkoani humo kutengeneza mazingira salama ya uwekezaji na kuweka mikakati ya kuwashawishi wawekezaji wawekeze katika maeneo yao.

Ametoa agizo hilo katika kikao cha wadau wa maendeleo mkoa humo cha kupokea taarifa ya tafiti ya fursa za uwekezaji kutoka TIRDO.

Amesema Manyara iko nyuma kimaendeleo kutokana na viongozi kusubiri wawekezaji waje bila kuwashawishi na kuwawekea mazingira salama ya uwekezaji ya utoaji wa leseni na hati.

"Mhakikishe mnabadilisha namba za simu na wawekezaji kushawishi wawekezaji. Msisubiri mwekezaji aje, inatakiwa wewe ukamshawishi ili aone fursa za uwekezaji," amesema.

Mnyeti amesema, serikali ya mkoa iko tayari kushirikiana na wawekezaji watakaofuata taratibu na sheria kwa kusikiliza wanasema nini kuhusu utoaji wa leseni na hati kupitia wakurugenzi watendaji wa halmashauri kuondoa urasimu usio wa lazima.

“Mwekezaji anataka kwenda kwenye eneo lake na gharama analipa lakini hamtaki kupima kwa sababu mnataka chochote. Nendeni mkatusaidie kukutana na kuwaelimisha watumishi wenu ili hili lisitokee," amesema.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa alikiruhusu kiwanda cha Malt Superbrand Limited mkoani humo kuendelea na uzalishaji wa bidhaa za vinywaji baada ya kufungwa na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa madai ya kuwa hawana kibali cha kutumia kemikali ambazo zinatumiwa katika utengenezaji wa bidhaa zao.

Ni miezi mitatu imefika tangu kiwanda hicho kilichokuwa kikizalisha vinywaji aina ya Sed na Strong Dry Gin kifungwe ambapo Mkurugenzi Mtendaji, David Mlokozi alisema waliomba kibali cha kutumia kemikali hizo hivi karibuni.

"Sisi tunatumia kemikali ya ndani. Tunanunua katika kiwanda cha Kifaru Mwanga. Kilimanjaro Bayokemi. Ni kemikali ya ndani na kuna watu wananufaika nayo," alisema Mlokozi.

Akizungumzia madhara ya kiwanda hicho baada ya kufungwa kiwanda hicho alieleza hawakuwa sokoni kwa miezi mitatu kuanzia Aprili mwaka huu. Hali hiyo inawapa nafasi kubwa washindani wanaotengeneza bidhaa kama zao.

Aliwalaumu waliofunga kiwanda hicho ambao ni Mkemia Mkuu wa serikali kuwa lengo lake lilikuwa ni wao kutokuwepo sokoni ili waweze kudhoofika na washindani wao kukua zaidi.

Aliwataka wanasiasa kutokuingilia michakato ya uanzishwaji wa viwanda kutokana na kile kilichoelezwa na wawekezaji kuwa wamekuwa wakikwamishwa na wanasiasa wanapoanza.

HIFADHI ya Taifa ya Ruaha imejipenyenza katika vyuo vikuu 20 ...

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Babati

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi