loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwanasoka England kujenga studio, kiwanda Tanzania

MCHEZAJI wa klabu ya Swansea ya England, Wilfred Bony amesema anavutiwa na wimbo wa Chura ulioimbwa na msanii, Snura Mushi.

Bony raia wa Ivory Coast ambaye alikuwa nchini kwa ziara binafsi alisema anaupenda wimbo wa Chura na anapenda kuusikiliza kutokana na jinsi mwanadada huyo anavyocheza.

“Chura ni wimbo mzuri kuangalia na ni mzuri kuusikiliza na video yake inavutia sana wanaume kwani wanaangalia jinsi wanawake wanavyocheza,” amesema Bony.

Pia alisema anavutiwa na kazi za sanaa zinazofanyika nchini na ameamua kuwekeza kwenye ujenzi wa studio ya kisasa, maktaba ya muziki na kiwanda cha filamu.

“Navutiwa na kazi za sanaa za Tanzania hasa muziki japokuwa nyingi zimetumia lugha ya Kiswahili, nazipenda nyimbo za Tanzania pia nazijua na huwa nazifuatilia sana.

“Wengi wanaweza kushangaa kwa kuwekeza kwangu katika sanaa ya filamu na muziki badala ya soka, haya ni mapenzi yangu kwa muziki na filamu baadaye naweza kufikiria kuwekeza katika soka,” amesema Bony.

Bony amefanya ziara ya utalii katika hifadhi na mbuga za wanyama nchini pia ametembelea vivutio vingine vya utalii nchini ikiwemo visiwa vya Zanzibar.

Bony mwenye umri wa miaka 29 kabla ya kutua Swansea City amewahi kucheza katika Klabu za Sparta Prague, Vitesse, Manchester City na Stoke City.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi