loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ufaransa yaing’oa Argentina

KYLIAN Mbappe ameipeleka Ufaransa robo fainali ya kombe la Dunia baada ya kinda huyo wa klabu ya Paris Saint-Germain kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Argentina jana.

Ushindi huo wa Ufaransa unahitimisha ndoto ya nyota wa Barcelona, Lionel Messi kushinda taji hilo na kuwa mmoja wa wachezaji bora wa muda wote katika historia ya mchezo wa soka. Messi aliyeiongoza Argentina kufika fainali ya kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil na kufungwa bao 1-0 na Ujerumani, aliisaidia timu yake kufika hatua ya mtoano kwa kufunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria wiki iliyopita.

Ufaransa walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti likiwekwa kimiani na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Greizmann baada ya Marcos Rojo kumuangusha Mbappe kwenye eneo la penalti. Angel Di Maria akaisawazishia Argentina dakika ya 41 na Barcadi kuifungia Argentina bao la pili dakika ya 48 na beki wa Ufaransa, Pavard akasawazisha dakika ya 57.

Kylian Mbappe aliifungia Ufaransa mabao mawili dakika ya 64 na 68 lakini mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero akaifungia Argentina bao la tatu kwenye dakika nne za nyongeza za mchezo huo. Kutokana na ushindi huo, Ufaransa itakutana na mshindi kati ya Ureno na Uruguay waliotarajiwa kucheza jana usiku.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi