loader
Picha

Uchumi Zanzibar wazidi kuimarika

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Zanzibar iko vizuri katika ukusanyaji wa mapato, hatua ambayo imefanya uchumi wake uendelee kuimarika siku hadi siku.

Aliyasema hayo, Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati ilipowasilisha utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2017/2018 na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa mwaka 2018/2019.

Alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na watendaji wake wote, kwa juhudi kubwa za ukusanyaji wa mapato na kueleza matumaini yake makubwa aliyonayo kwa wizara hiyo.

Alisisitiza haja kwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari wakati changamoto zinapojitokeza katika utoaji wa huduma zake za fedha.

Alisema ikilinganishwa na miaka ya nyuma, kwa kiasi kikubwa Zanzibar imepunguza kuwatumia wataalamu wa nje katika kuendesha miradi yake ya maendeleo na kazi nyingi katika wizara za serikali hivi sasa zimekuwa zikifanywa na wataalamu wazalendo, hali inayoonesha tofauti kubwa na nchi nyingi za bara la Afrika.

Ametoa mwito kwa Wizara ya Fedha na Mipango kutonyamaza kimya kwani mapato ya Zanzibar yameimarika hivyo, ipo haja kwa wananchi kuyajua mafanikio hayo sambamba na mikakati iliyowekwa na serikali katika kuhakikisha mapato yake yanaimarika.

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee aliupongeza uwasilishaji Mpango Kazi na utekelezaji wake uliofanywa na wizara hiyo na kusisitiza haja ya usimamizi wa majukumu yao pamoja na kuwasimamia watendaji walio chini yao ili kuepuka udhoroteshwaji wa malengo yaliokusudiwa.

Mapema Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed, alisema kuwa Uchumi wa Zanzibar umeendelea kuimarika na wenye kutoa taswira ya matumaini mazuri mwaka hadi mwaka.

Alieleza kuwa kwa mwaka 2017, Pato la Taifa limeongezeka na kufikia Sh bilioni 1,363 ikiinganishwa na Sh bilioni 1,268 kwa mwaka 2016.

HIFADHI ya Taifa ya Ruaha imejipenyenza katika vyuo vikuu 20 ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi