loader
Picha

TRC yafungua biashara Uganda

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limepania kurahisisha usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki na nchi nyingine za karibu.

Wiki iliyopita TRC ilirejesha safari za treni za mizigo kutoka Tanzania mpaka Kampala Uganda kupitia Tabora, Isaka, Mwanza na Ziwa Victoria kwa kutumia bandari ya Mwanza na Port Bell nchini Uganda.

Hatua hiyo imefanyika baada ya kusitishwa kwa usafiri huo kwa miaka 10, jambo ambalo kurejeshwa kwake kutaleta manufaa ya kiuchumi kwa nchi hizo mbali na wananchi wake.

Urejeshwaji wa safari hiyo, unaendeleza nyingine za wateja wao wakubwa ambao ni Burundi na Jamhuri ya Kidemokarasia ya Kongo (DRC) huku wakiwa na mipango ya kufufua njia za kupeleka mizigo katika nchi za Kenya na Rwanda ambako kwa sasa mizigo imeshuka.

Akizungumza katika banda la shirika hilo lililopo katika maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa,kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Ofisa Uhusiano wa shirika hilo Jamila Mbaruk, alisema usafirishaji wa mizigo katika nchi hizo kwa kutumia treni utasaidia katika kuboresha biashara za wafanyabiashara wa pande zote.

Amesema licha ya unafuu wa bei katika kusafirisha mizigo, usalama ni wa uhakika kwani mizigo inasindikizwa na askari kwa behewa moja kubeba tani 40 hadi 42 wakati barabara mizigo ni tani 30 pekee.

Pia alibainisha kuwa ikiwa treni ambayo ni nadra kupata ajali lakini itatokea mteja ataitwa katika eneo la ajali kasha kulipwa fedha ya hasara ya bidhaa zake.

Alisema takribani tani 15,000za mizigo ikijumuisha, mafuta ya kula, unga na maharage kutoka shirika la mpango wa chakula duniani (WFP)zinatarajia kusafirishwa hadi mwisho wa mwezi huu kuelekea nchini Uganda.

Juni 24 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alifungua safari za treni za mizigo kuelekea nchini Uganda akishuhudiwa na wakazi mkoa wa Mwanza, na treni ya kwanza ya mizigo iliingia katika meli ya mizigo ya Mv Umoja katika bandari ya Mwanza ili kuvushwa ziwa Victoria kwenda nchini Uganda.

Kaimu mkurugenzi wa Uendeshaji wa TRC, Focus Sahani alisema kuanza kwa safari hiyo ni maelekezo ya rais John Magufuli alipofanya ziara Uganda akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kuwataka wakurugenzi wa TRC, Mamlaka ya bandari (TPA) na watoa huduma za maji kuhakikisha njia hiyo inafunguliwa.

Alisema baada ya agizo hilo waliwapatia vifaa Uganda ili waweze kufungua njia yao ya kilometa tisa iliyokuwa kikwazo na kushukuru serikali kwa kuwawezesha kupata vichwa vya treni hizo za mizigo.

Mkuu wa kitengo cha logistiki kutoka WFP, Mahamud Mabuyu alisema wameamu kutumia usafiri huo kusafirisha mizigo yao kutokana na gharama nafuu pamoja na kuvutiwa na huduma za shirika hilo mwaka jana walipotumia reli kusafirisha mizigo tani 16 kwenda Dodoma na Isaka na hakuna mzigo uliopotea.

HIFADHI ya Taifa ya Ruaha imejipenyenza katika vyuo vikuu 20 ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi