loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sweden yatia timu robo fainali

EMIL Forsberg jana alifunga bao lililoipeleka Sweden robo fainali za kombe la dunia katika mechi ya hatua ya 16 dhidi ya Uswisi. Katika mechi hiyo ambayo Sweden ilishinda bao 1-0 lililofungwa dakika ya 66, beki wa Uswisi Manuel Akanji akiwa katika harakati za kuokoa akajikuta akisaidia kuupeleka mpira kwenye nyavu za timu yake huku kipa wake Yann Sommer akibaki anautazama.

Michael Lang wa Uswisi alitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 90 kwa kumfanyia madhambi Martin Olsson. Sweden sasa itacheza na mshindi wa mechi kati ya England na Colombia iliyotarajiwa kuchezwa jana usiku. Ikiwa imekosa nafasi kadhaa za wazi za kufunga, Andreas Granqvist aliokoa mpira wa kichwa wa Breel Embolo uliokuwa ukielekea golini na mchezaji wa akiba Remo Freuler aliokoa hatari katika dakika za majeruhi Uswisi ilipokuwa ikihaha kusaka bao la kusawazisha.

Sweden ambayo mara ya mwisho ilivuka hatua hiyo mwaka 1994 ilikuwa ipate bao la mapema katika kipindi cha kwanza lakini Albin Ekdal shuti lake lilipaa lango. Jambo la kusikitisha katika mechi ya jana ni nyota wa Sweden, beki wa Celtic Mikael Lustig kuoneshwa kadi ya pili ya njano hivyo atakosa mechi ya robo fainali.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi