loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha Ubelgiji atumia mbinu mbadala

KOCHA wa Ubelgiji, Roberto Martinez ilibidi kutumia mbinu mbadala baada ya timu yake kuwa nyuma ya mabao 2-0 dhidi ya Japan katika mchezo wa Kombe la Dunia hatua ya 16 bora. Japan ilionesha soka safi na kuifunika Ubelgiji, lakini kocha Martinez alibadili mbinu za kiufundi na kuiwezesha timu yake kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na kukata tiketi ya kucheza robo fainali.

Kwa ushindi huo, Ubelgiji sasa itakutana na mabingwa mara tano wa dunia, Brazil katika mchezo wa robo fainali. Baada ya kipindi cha kwanza, wakati kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji kilipolosa bahati na kusubiri hadi dakika za mwisho kupata ushindi huo baada ya kocha wao kuwatoa baadhi ya wachezaji na kuwaingiza wengine.

Wiki iliyopita kulikuwa na mdahalo kuhusu kama Ubelgiji au England nani atajikuta katika nafasi ratiba rahisi baada ya timu hizo kufuzu kwa raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia. Baada ya mambo kuwa magumu, kocha wa Ubelgiji aliligeukia benchi lake la ufundi na kufanya mabadiliko kadhaa, ambayo yalionesha wazi kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi huo wa ajabu.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi