loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Salah asaini mkataba mpya Liverpool

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah amesaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuichezea klabu hiyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na klabu hiyo akitokea AS Roma kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 34 katika kipindi cha majira ya joto kilichopita na amefunga mabao 44 katika mechi 52 alizoichezea klabu hiyo.

Mkataba huo, ambao utamwezesha mchezaji huyo kuwepo Liverpool hadi mwaka 2023, hauko wazi, lakini inadaiwa kuwa Salah ambaye alikuwa akilipwa pauni 100,000 kwa wiki, sasa ataweka kibindoni zaidi ya pauni 200,000 kwa wiki.

"Hii inaelezea wazi mambo mawili, anaamini katika Liverpool na sisi tunamwamini yeye,"alisema kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Salah alikuwa mfungaji wa mabao mengi katika Ligi Kuu msimu uliopita, baada ya kupachika mabao 32 – katika mechi 38 alizoichezea klabu hiyo na kumwezesha kupata kiatu cha dhahabu.

Kiwango chake pia kilimwezesha mchezaji huyo kupata tuzo ya mwaka ya mwanasoka bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa.

"Nimefurahi kubaki na kusaini mkataba mwingine mpya katika klabu hii," alisema mchezaji huyo.

"Mwaka wangu wa kwanza katika klabu huu ulikuwa na uzoefu wa aina yake kwangu na kwa familia yangu. Namshukuru kila mtu katika klabu hii pamoja na mashabiki. "Najua tutafanikiwa mengi pamoja katika klabu hii.”

Liverpool ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita na kufungwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Real Madrid kwa mabao 3-1.

Salah ilibidi kutoka mapema baada ya nusu saa tangu kuanza kwa mchezo huo wa fainali dhidi ya vigogo Real Madrid katika mchezo uliofanyika Kiev baada ya kuumia bega.

Matatizo hayo yalimfanya ushiriki wake wa Kombe la Dunia kuwa katika wasiwasi na alikosa mchezo wa ufunguzi wa Misri dhidi ya Uruguay, ambako walifungwa 1-0, kabla ya kuanza walipocheza dhidi ya Urusi na Saudia Arabia.

Salah alifunga katika mechi hizo zote, lakini haikuzuia nchi yake kuondolewa mapema katika Kombe la Dunia katika hatua ya makundi ya mashindano hayo.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi