loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

England yatinga nusu fainali

ENGLAND jana imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya miongo kadhaa baada ya kuifunga Sweden kwa mabao 2-0. Bao la kwanza la England liliwekwa kimiani katika dakika ya 30 na Harry Maguire kwa kichwa akiunganisha wavuni mpira wa kona katika mchezo huo war obo fainali.

Maguire ambaye ni beki wa kati aliunganisha kona iliyochongwa na Ashley Young na kufunga bao lake la kwanza katika mchezo wa kimataifa na kuiweka England katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Kwa ushindi huo, England sasa itacheza ama na wenyeji Urusi au Croatia, ambao walitarajia kucheza jana usiku katika mchezo war obo fainali ya pili nchini Urusi.

England kwa mara ya mwisho ilicheza hatua hiyo ya nusu fainali mwaka 1990 na sasa kikosi chake chipukizi kimefanikiwa kutua katika hatua hiyo chini ya kocha Gareth Southgate. Bao la pili la England lilifungwa na Dele Alli kwa kichwa katika dakika ya 58 ya mchezo huo na kuihakikishia England ushindi. Tayari Ubelgiji imefuzu nusu fainali baada ya kuifunga Brazil 2-1 na Ufaransa ishinda 2-0 na kutinga katika hatua hiyo.

Vikosi vilikuwa: Sweden (4-4-2): Robin Olsen; Emil Krafth, Victor Lindelof, Andreas Granqvist (nahodha), Ludwig Augustinsson; Viktor Claesson, Sebastian Larsson, Albin Ekdal, Emil Forsberg; Marcus Berg na Ola Toivonen. England (3-5-2): Jordan Pickford; Kyle Walker, John Stones, Harry Maguire; Kieran Trippier, Ashley Young, Jordan Henderson, Jesse Lingard, Dele Alli; Raheem Sterling na Harry Kane (nahodha).

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi