loader
Picha

Waafrika waiunga mkono Ufaransa

MIOYO ilivunjika wakati mataifa yote matano ya Afrika, Senegal, Nigeria, Misri, Morocco na Tunisia – kutolewa katika hatua ya kwanza ya mashindano ya Kombe la dunia, lakini baadhi ya mashabiki wanasema hawajapoteza matumaini. “Angalau bado tuna timu ya taifa ya Ufaransa, “ watu wengi walitania katika mitandao ya kijamii.

Hata Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron naye aliingia katika utani, pale alipowaambia Wanigeria juzi kuwa sasa Super Eagles wametolewa katikamashindano ya Kombe la Dunia, inabidi waishangilie Ufaransa. Ni kweli, timu ya taifa ya Ufaransa ina wachezaji 14 katika kikosi chake, ambao wanaweza kuchezea nchi za Afrika.

Wachezaji wawili wa Ufaransa wenye undugu wamefanya hivyo. Kaka yake Paul Pogba, Florentin, anachezea Guinea, wakati kaka yake Steve Mandanda, Parfait, yeye anachezea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wote awali walikuwa wakiichezea timu za taifa za vijana za Ufaransa kabla ya kuamua kuzichezea timu, ambako wazazi wao wanakotoka. Nyota wa sasa wa Ufaransa katika mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia, mwenye umri wa miaka 19, Kylian Mbappé, alizaliwa na baba Mcameroon na mama Mfaransa.

Wakati huohuo, Ubelgiji ina wachezaji nane wenye asili ya Afrika, ambapo mmoja kati ya wazazi wao ama baba au mama au wote wanatoka katika bara hilo, Katika kikosi hicho kuna wachezaji kama akina Kompany, Fellaini, Lukaku, Dembélé, Boyata, Batshuayi, Chadli na Tielemans. SHERIA ZA FIFA Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) liliweka sheria na taratibu za mchezaji kuweza kuchezea taifa jingine: Wacheza soka ambao wanacheza mashindano ya kishindani ya kimataifa katika timu moja hawawezi kuhamia katika timu ya taifa jingine. Lakini sheria hii ilirahisishwa na kuwawezesha wanasoka kubadili utaifa kutoka katika timu ya vijana hadi ileya wakubwa.

Mechi za kirafiki hazizuii, hivyo Diego Costa aliweza kuhamia Hispania baada ya kucheza mechiza kirafiki za kimatifa akiwa na timu ya taifa ya Brazil, kama alivyofanya mchezaji wa Ubelgiji Nacer Chadli baada ya kuichezea mchezo wakirafiki timu ya taifa ya Morocco. Wachezaji ambao hawana uhusiano wa kidamu na nchi, waliruhusiwa tu kuwakilisha nchi hiyo ikiwa tu watakuwa wameishi na kucheza soka katika nchi hiyo kwa miaka mitano. Lakini hilo ni tofauti kabisa na wakimbizi, ambao wanaweza kuichezea nchi wanayoishi kama wakimbizi bila ya kuishi pale kwa miaka mitano. SWEDEN NA KENYA Pia waliondoka katika mashindano ni pamoja na England, Sweden, Uruguay, Brazil, Urusi na Croatia.

Wachezaji wenye wazazi wa Afrika katika kikosi cha England ni Delle Alli – ambaye baba yake anatokea Nigeria na mchezaji mwenzake Danny Welbeck ambaye alizaliwa Manchester na wazazi wa Ghana. Msweden, John Guidetti aliishi Kenya kwa miaka mitatu akiwa mtoto, akionesha kipaji chake akiwa na timu ya watoto ya Nairobi iliyoshiriki Lig Ndogo. Mashabiki wa Kenya walifurahia kubadilishana picha katika mitandao ya kijamii ya chipukiuzi Guidetti. “Bado nina uhusiano mkubwa na Kenya na kila wakati ninarudi nchini humo na kupata mapokezi makubwa, “alisema Guidetti akikaririwa na gazeti la Standard.

Kocha wazamani wa Guidetti, Chris Amimo, aliliambia gazeti hilo kuwa Guidetti “wakati wote amekuwa akipangwa katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Kenya. Anapenda kucheza. “Baba yake anafanyakazi katika shule ya Sweden, ambayo iko jirani kabisa na uwanja wa Ligi Ndogo, “alionsema. Wakati Guidetti ambaye anaangukia katika sheria hizo za Fifa, mchezaji mwenzake wa Sweden Martin Olsson alizaliwa na mama Mkenya na kinadharia ana nafasi ya kuchagua moja kati ya nchi hizo. “Wachezaji wengi wa kulipwa ambao wamethibitishwa kucheza soka la kiamtaifa, wanacheza Ulaya…” “Ni kweli sita kati ya wachezaji 23 katika kikosi cha Morocco waliocheza fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia, walizaliwa katika nchi hiyo.”

MUIGIZAJI wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuna uwezekano wa ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi