loader
Picha

Ufaransa yatamba kuifunga Ubelgiji

UFARANSA itacheza nusu fainali dhidi ya majirani zao wa Ubelgiji ikiwa na “njaa ya ushindi” kwa lengo la kumuonesha bingwa wao wa Kombe la Dunia 1998, Thierry Henry kuwa, uamuzi wake wa kuifundisha Ubelgiji sio sahihi, alisema jana mshambuliaji Olivier Giroud.

Henry ni mchezaji wa kimataifa wa soka mstaafu wa Ufaransa, ambaye sasa ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji. Timu hizo mbili zinakutana kesho katika mchezo utakaoamua nani atacheza fainali ya Kombe la Dunia Julai 15.

"Ni kioja kuwa na Thierry dhidi yetu katika mchezo huu", alisema Giroud alipozungumza na waandishi wa habari.

“Nitajivunia sana kumuonesha Thierry kuwa amechagua kambi isiyo sahihi.”

Timu zote zilianza mashindano haya zikiwa hazipewi kabisa nafasi ya kufanya vizuri katika Kombe la Dunia mwaka huu, huku Ufaransa ikiifungisha virago Uruguay katika robo fainali na Ubelgiji iliwatoa mabingwa mara tano na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali.

"Nilikuwa napendelea tungekuwa na Henry upande wetu, ili kunipa ushauri mimi na washambuliaji wengine wa Ufaransa, lakini huo sio wivu," alisema Giroud mwenye umri wa miaka 31.

Mshambuliaji huyo alikuwa akikosolewa na Henry huko nyuma, lakini hakuwa na tatizo jingine zaidi ya kuwa na kiu ya kushinda.

"Imekuwa ni miaka michache tangu aliposema kuhusu mimi. Kazi yangu huwa nzuri kiwanjani, kuliwakilisha Ufaransa inavyowezekana. Hiyo pia ni mechi maalum kwa ajili yake. "Kwa kweli nataka kuwasiliana (na wachezaji wenzangu) hamu yangu ya kushinda.”

Mchezo ninaotarajia utatawala kurasa za mbele za nchi zote mbili, zikikamilishwa na nukuu za asili za vitabu vya muda mrefu vya vikatuni.

"Kwa kweli ni zaidi ya mechi,"ilieleza Aujourd’hui gazeti moja ya Ufaransa lilieleza katika ukurasa wake mzima wa mbele, ambalo liliweka picha za vibonzo maarufu vya nchi hizo mbili - Tintin kwa Ubelgiji na Asterix kwa Ufaransa.

Giroud alisema wachezaji wenzake wanaijua vizuri timu ya Ubelgiji, huku wachezaji wake wengi kutoka timu zote mbili wanacheza katika Ligi Kuu ya Uingereza, akiwemo yeye mwenyewe.

Lakini alisema Ufaransa ina wachezaji wengi wenye vipaji na uzoefu mkubwa kuiangusha safu ya ulinzi ya Ubelgiji na kumfunga kipa Thibaut Courtois.

"Courtois ni mchezaji mzuri. Ni mchezaji katika Kombe hili la Dunia ikiwa na safu safi ya ulinzi, " alisema Giroud.

"Kutakuwa na nafasi, ambayo sisi tutaitumia kuwafunga," aliongeza mshambuliaji huyo. "Ninashawishika kusema kuwa tutavunja ukuta huo.”

MCHUANO mkali wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya hatua ya ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi