loader
Picha

Ubelgiji Vs Ufaransa lazima kieleweke

NUSU fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la dunia inachezwa leo ambapo Ubelgiji itamenyana na Ufaransa katika mechi inayotarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee.

Ubelgiji imetamba kuibuka na ushindi katika mechi hiyo itakayochezwa leo saa tatu usiku. Kocha Mkuu wa timu hiyo, Roberto Martinez alisema kuwa timu yake iko vizuri na ana matumaini makubwa kuwa leo wataibuka na ushindi na kutinga fainali ya michuano hiyo itakayochezwa Jumapili ya wiki hii.

Kikosi hicho cha Martinez kinakabiliana na mabingwa wa Dunia wa mwaka 1998 katika mchezo utakaochezwa jijini St Petersburg katika mbio za kuwania nafasi ya kucheza fainali.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ubelgiji kufikia hatua hii ya michuano ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1986, walipomaliza katika nafasi ya nne.

"Wachezaji wako pamoja kwa kipindi kirefu na wanastahili kuwepo hapa walipo leo,” amesema kocha huyo.

"Nafikiri kitu muhimu tulichofanya ni kuhakikisha timu inakuwa pamoja kwa muda mrefu na inacheza kitimu, mbinu binafsi na kipaji ni muhimu, lakini mashindano haya, ni muhimu kucheza kitimu.

"Ni safari ya kuelekea kusikojulikana. Hatujawahi kuwepo katika hali kama hiyo, na ndio sababu tunahitaji ari ya kitimu zaidi dhidi ya Ufaransa. Tunatakiwa kuwa katika hali nzuri zaidi.”

Kocha anaona usawa kati ya Ubelgiji na wapinzani wetu, hasa wakati linapokuja suala la utajiri wa kipaji cha mchezaji mmoja mmoja katika viwango vyao. Ubelgiji inajivunia wakali wake kama Romelu Lukaku, Eden Hazard na Kevin De Bruyne, wakati Antoine Griezmann na Kylian Mbappe wataonesha njia kwa upande wa Ufaransa katika mchezo huo nchini Urusi.

Mbappe alikuwa mwiba mkali Ufaransa iliposhinda 4-3 katika raundi ya 16 bora dhidi ya Argentina, lakini Martinez alisema kuwa hawatafanya makosa kumuangalia mchezaji mmoja.

"Timu nzima ina mchanganyiko sahihi wa vijana na wachezaji wenye uzoefu napia imejaa vipaji binafsi,” aliongeza. "Kundi letu la wachezaji linahitaji kucheza bila hofu ili kuweka mchezo kuwa wazi, hilo litatufanya tushinde.”

MCHUANO mkali wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya hatua ya ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi