loader
Picha

Kiungo Mkenya aahidi raha Simba

KUTOKANA na kuwepo kwa tetesi kuwa Simba SC inamnyatia kiungo wa Gor Mahia, Francis Kahata, kiungo huyo amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa waharakishe dili hilo ili aanze kuwapa raha.

Simba ambao wametinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Kagame linaloendelea, Dar es Salaam kwa sasa, tayari imeshawanasa wachezaji Maddie Kagere, Adam Salamba, Marcel Kaheza, Mohammed Rashid na Pascal Wawa ambao watawatumia kwenye ligi pamoja na mashindano mengine watakayoshiriki.

Kahata amesema amekuwa akizisikia taarifa za kutakiwa na Simba na amezipokea kwa furaha kubwa hivyo anasubiri kuona hatima yake.

Alisema kama dili hilo litakamilika basi atakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo kutokana na kufahamu kuwa mashabiki wa timu hiyo hakuna wanachokihitaji kwa sasa zaidi ya mataji.

Alifafanua kuwa yeye ana wakala ambaye ndiye anamsimamia mambo yake yote hivyo Simba lazima wapitie kwa wakala huyo kama wanataka kurahisisha mambo.

“Nimekuwa nikisikia Simba wananitaka, siwezi sema hiyo ni timu mbaya nimeona mara kadhaa wamefanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa Afrika. Mimi nina wakala wangu kama mambo yatakwenda vizuri sina kipingamizi nitakuja Simba.

“Nitafurahi kucheza Simba maana nitakutana na Meddie (Kagere) ambaye nimekuwa nikicheza naye Gor Mahia na kupata mafanikio, timu hiyo ina wachezaji wazuri na kiukweli nitafurahi kuichezea Simba,” alisema Kahata.

MUIGIZAJI wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuna uwezekano wa ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi