loader
Picha

Mauzo ya EAC Ulaya yapaa kwa bil. 400/-

THAMANI ya mauzo ya bidhaa za Afrika Mashariki katika Umoja wa Ulaya (EU) yameongezeka hadi Dola za Marekani bilioni 2.5 (Sh trilioni 5.2 za Tanzania) mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia nane.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC).

Kwa mujibu wa ITC, bidhaa kutoka ukanda huo zilizouzwa Ulaya kwa mwaka 2016 zilikuwa na thamani ya Dola milioni 2.3 (Sh trilioni 4.83 za Tanzania), hivyo kumekuwa na ongezeko la takribani Sh bilioni 400.

 Mkurugenzi wa Sekta ya Uzalishaji ya EAC, Jean Baptiste, amesema hivi karibuni jijini Arusha yalipo makao makuu ya jumuiya hiyo kuwa, ili kuliteka zaidi soko la EU, ukanda wa Afrika Mashariki unapaswa kuelekeza nguvu katika ubora utakaokwenda sambamba na ule wa Ulaya.

Miongoni mwa bidhaa za EAC zenye soko katika jumuiya ya Ulaya ni pamoja na kahawa, maua, chai, pamba, samaki na mboga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC), Lillian Awinja, alisema suala la maridhiano katika biashara baina ya EU na EAC linahitajika haraka ili kuzisaidia nchi za Afrika Mashariki kuongeza mauzo yake nje.

“Tunahangaika na sekta binafsi katika ukanda wetu kuzitaka ziongeze uzalishaji wa bidhaa na kuzijaza katika soko letu, kuongeza uzalishaji wa bidhaa zenye ushindani ndani ya jumuiya na kimataifa pia. Kutoka hapo, tutaweza kutamba kila kona….,” amesema.

HIFADHI ya Taifa ya Ruaha imejipenyenza katika vyuo vikuu 20 ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi