loader
Picha

Vifo vya ajali vyapungua Dodoma

MKOA wa Dodoma umefanikiwa kupunguza matukio ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa asilimia 14 hadi Juni mwaka huu.

Ajali hizo zimepungua kutoka 91 katika mwaka 2017 hadi 49 katika mwaka huu, huku vifo vikipungua kutoka 69 hadi 37 katika kipindi hicho hicho.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Swalehe Digega amesema, kupungua kwa vifo hivyo kunatokana na mipango madhubuti iliyowekwa na jeshi hilo.

Amesema jeshi hilo limeweka mikakati mingi, ikiwemo ya kuhakikisha madereva wanatii sheria za usalama barabarani bila shuruti, kutoa elimu katika mikusanyiko ya watu na kwa wadau mbalimbali wa usalama barabarani.

Digega amesema mafanikio hayo ya kupunguza vifo barabarani pamoja na ajali yametokana pia na kufanya msako wa makosa mbalimbali wa makosa ya usalama barabarani pamoja na kudhibiti mwendokasi wa magari kwa kutumia vidhibiti mwendo.

Amesema miongoni mwa sababu zinazochangia ajali za barabarani ni madereva wa pikipiki kutotumia kofia ngumu kwa ajili ya kuzuia madhara pindi ajali inapotokea.

"Pamoja na mtindo wa kupakia watoto wenye umri wa chini ya miaka tisa hali ambayo kwa mkoa huu ilikuwa likitiliwa mkazo,"amesema.

Digega alisema jeshi hilo limekuwa likifanya operesheni ya kushtukiza katika barabara ya Dodoma- Morogoro na wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara.

"Katika ukaguzi huo wa mara kwa mara, wamebaini ukiukwaji wa sheria kwa uzembe au makusudi, ulevi wa makusudi na uelewa duni wa masuala ya usalama barabarani,"amesema.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Marrison Mwakyoma amesema suala la usalama ni la wote, hivyo kila mmoja anayevunja sheria anakamatwa.

Rais John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi