loader
Picha

Watoto wote 12, mwalimu waokolewa

Hatmaye juhudi za kuwaokoa watoto wote 12 pamoja na kocha wao waliokuwa wamekwama kwenye pango la Tham Luag lenye urefu wa kilomita 10, zimefanikiwa jana.

Kabla ya jana, watoto wanane walikuwa tayari wameokolewa kwa siku mbili za mwanzo na waliwahishwa hospitalini kwa uchunguzi ikiwemo kuchukuliwa vipimo vya X-ray na damu, lakini pia wamewekwa kwenye karantini kuzuia kama kunaweza kutokea maambukizi yoyote. Taarifa kutoka katika hospitali walikolazwa zinasema kuwa watoto wawili kati ya hao wanane waliokuwa wamekwishaokolewa, waligundulika kuwa na dalili za homa ya mapafu na wameanzishiwa dozi ya ya ugonjwa huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini humo, Jedsada Chokdamrongsuk, alisema kuwa kwa ujumla vijana hao wanaendelea vizuri kiafya na wanakula vizuri, ingawa wawili kati yao ndiyo walionekana kuwa na shida kwenye upumuaji. Alisema hali hiyo inaweza kuwa ilisababishwa na kunywa maji machafu au kunyewa na ndege au popo kitu ambacho kinaweza kusababisha maambukizi hatari. Watoto wote waliookolewa wamevalishwa miwani ya jua ili kuwakinga na mwanga wa jua, lakini pia wote wamepungua uzito.

Njia iliyokuwa ikitumiwa na waokoaji hao ni wapigambizi wawili kumuokoa mtoto mmoja ambapo mpiga mbizi mmoja alikuwa mbele, mtoto mmoja katikati na mpigambizi mwingine nyuma. Watoto wanne na mwalimu waliokolewa jana. Imeelezwa kuwa ingawa uokoaji kwa siku ya jana ungeweza kuchukua muda mrefu zaidi, lakini waokoaji walidhamiria kuwaokoa watoto wote, kocha wao pamoja na daktari aliyekuwa akiwahudumia huko pangoni. Hewa ya oksijeni iliendelea kupelekwa kwa wingi ndani ya pango hilo ili kuhakikisha uhai wa wote walioko ndani ya pango hilo unakuwa salama.

“Kama hali ya hewa haitabadilika, tunategemea watoto wote wanne, kocha wao, daktari na wapigambizi watatu waliokuwa na watoto hao tangu siku ya kwanza, wataokolewa leo,”alieleza Narongsak.

Wakumbukwa na wenzao

Kabla ya watoto hao kuokolewa wote, waliotangulia kuokolewa walianza kuwakumbuka wenzao walionasa pangoni na kuwatakia afya njema. Mmoja wa watoto hao, Phansa Namyee, alitoa wito kwa watoto wenzake kuokolewa haraka ili waendelee na masomo, lakini pia aweze kucheza nao na kupata chakula nao mgahawani.

Kwa nini walikwenda pangoni?

Mmoja wa waokoaji alisema kuwa inawezekana watoto hao walikwenda pangoni humo kwa ajili ya kufanya ibada au mila maalumu. Alisema kuwa vijana hao walivua viatu na kuacha mabegi yao nje ya pango hilo. “Kabla hawajaingia pangoni, inaonekana kama kuna mila ambayo hufanyika pangoni kwa vijana kama hao wa kiume, kwa sababu walivua viatu na kuacha mabegi yao nje ya pango, lakini moja ya mambo wanayofanya ni kuandika majina yao kwenye kuta za pango hilo,”alieleza mmoja wa waokoaji hao. Hata hivyo, vyanzo vingine vinasema kuwa walikwenda pangoni humo kama sehemu ya burudani au kuburudisha akili.

Waandika barua

Ijumaa iliyopita, watoto hao waliwaandikia barua wazazi na marafiki zao na kuwahakikishia kuwa wako salama. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa watoto hao kuwasiliana na wazazi na marafiki zao tangu wanase kwenye pango hilo wiki tatu zilizopita. Kupitia barua hiyo iliyoandikwa kwa mkono, watoto hao waliwaomba wazazi wao chakula ikiwemo kuku waliokaangwa, huku kocha wao naye akiwaomba radhi wazazi wa watoto hao katika barua tofauti.

Aidha, mpaka Ijumaa iliyopita, zaidi ya lita milioni 130 za maji zilikuwa zimeshavutwa kutoka kwenye pango hilo na kazi hiyo ya kuvuta maji hayo iliendelea hadi jana.

Muda walionaswa pangoni

Watoto hao 12 wa kiume ambao ni wachezaji wa mpira wa miguu wenye umri kati ya miaka 11 na 16 pamoja na kocha wao mwenye umri wa miaka 25, walinasa chini ya pango hilo la Tham Luag tangu Juni 23 mwaka huu. Pamoja na juhudi hizo za kuwaokoa kuendelea, waokoaji walikabiliwa na changamoto ya giza na maji yanayoingia kwenye pango hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

 Mmoja wa waokoaji hao ambaye ni mwanajeshi mstaafu, Samarn Poonan (38), alikufa katika juhudi za kutaka kuwaokoa vijana hao baada ya kunasa chini ya pango hilo. Hatari nyingine ilikuwa ni kwamba miongoni mwa vijana hao, hakuna hata mmoja kati yao alikuwa na uwezo wa kuogelea. Kwa mujibu wa waokoaji, vijana hao walikuwa wanakabiliwa na njaa na walianza kudhoofika ingawa kiafya wako vizuri.

Rais John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa ...

foto
Mwandishi: BANGKOK, Thailand

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi