loader
Picha

Kumekucha nusu fainali Kagame

NUSU fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inatarajiwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Gor Mahia itacheza na Azam FC 8:00 mchana na Simba itaivaa JKU saa 11:00 jioni.

Katika mchezo wa robo fainali Simba iliifunga AS Ports ya Djibouti kwa bao 1-0 na JKU ikaifunga Singida United kwa penalti 4-3 baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana. Mabingwa watetezi Azam FC walifuzu nusu fainali kwa kuifunga Rayon Sports ya Rwanda kwa mabao 4-2 na Gor Mahia ya Kenya iliifunga Vipers ya Uganda kwa mabao 2-1.

Akizungumza jana Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholaus Musonye alisema michuano hiyo imefanikiwa kwa asilimia kubwa licha ya ratiba yake kuingiliana na Kombe la Dunia huku akiipongeza Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji.

“Naipongeza Tanzania kupitia Shirikisho la Soka, TFF, kwa kuwa mwenyeji wa mashindano haya kwani yamefanikiwa kwa asilimia kubwa licha ya ratiba yake kuingiliana na ratiba ya kombe la dunia,” alisema Musonye. Aidha Musonye alimshukuru Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa kufadhili mashindano hayo tangu mwaka 2002 kwa kutoa zawadi kombe na fedha kwa bingwa hadi mshindi wa tatu.

“Bingwa atapata dola za Marekani 30,000, mshindi wa pili dola 20,000, na mshindi wa tatu dola 10,000 na hizi zote zinatolewa na Rais Kagame pamoja na kikombe cha bingwa hivyo tunamsukuru sana,” alisema Musonye. Mashindano ya Kagame yalishirikisha timu 12 ambazo zilikuwa katika makundi matatu yenye timu nne kila moja. Kundi A lilikuwa na timu za Azam FC, Vipers, JKU na Kator FC, Kundi B lilikuwa na timu za Rayon Sports, Gor Mahia, Lydia Ludic na Ports na kundi C lilikuwa na Simba, Singida United, APR na Dakadaha. Fainali itachezwa keshokutwa, ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.

MUIGIZAJI wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuna uwezekano wa ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi