loader
Picha

Mawasiliano simu za mkononi yapenya 94%

SERIKALI imefanikiwa kuwafikishia Watanzania mawasiliano ya simu za mikononi kwa asilimia 94, amesema Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, amesema kuwa jukumu kubwa la UCSAF ni kuhakikisha Watanzania wanawasiliana.

Alisema kuwa kazi iliyobaki sasa ni kuhakikisha asilimia sita iliyobakia inapelekewa mawasiliano hayo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, amesema, Kamati yake imefika kwenye ofisi hizo za UCSAF kwa ajili ya kuangalia shughuli zinazofanywa na Mfuko huo.

"Mfuko huu umefanya kazi nzuri kwa sababu mpaka sasa umeshapeleka minara zaidi ya 530, wananchi wengi wanadhani kwamba minara mingi inayoonekana imejengwa na makampuni binafsi ya simu kama vile Vodacom, Airtel, Tigo na TTCL, lakini wafahamu kwamba minara zaidi ya 500 imetolewa na UCSAF," amesema Kakoso.

Alisema kuwa UCSAF imepeleka mawasiliano mahali ambapo makampuni binafsi yaliacha kupeleka mawasiliano hayo ya simu. Alisema minara iliyojengwa na mfuko huo inatumiwa na makampuni ya simu yaliyopo.

Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Dk Joseph Kilongola, alisema kuwa pamoja na mambo mengine, jambo linalofanywa na mfuko huo kwa sasa ni kuwahamasisha wawekezaji katika mitandao, huduma za posta, redio na televisheni kwenda kwenye maeneo ambako hakuna mvuto wa kibiashara.

Kwa maeneo ya mipakani, Dk Kilongola alisema kuwa UCSAF inahakikisha usikivu wa simu na redio unaongezeka ili wananchi wa huko wapate habari sahihi za hapa nchini badala ya kupata habari ambazo siyo sahihi kutoka nchi jirani.

Kwa mujibu wa Dk Kilongola, changamoto zinazoukabili mfuko huo kwa sasa ni uhaba wa fedha pamoja na takwimu zisizo sahihi kuhusu maeneo ambako yanapaswa kupelekwa mawasiliano.

Awali, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Peter Ulanga, alisema kuwa mpaka sasa wameshasaini mikataba ya kufikisha mawasiliano kwa kata 530 zenye vijiji 2,132 na wakazi wapatao milioni 3.6.

Alisema Kata 468 kati ya hizo 530 zenye vijiji 1,980 na wakazi milioni 3.2 zimeshapata huduma ya mawasiliano ambayo ni asilimia 88.

Rais John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi