loader
Picha

90% Kusini Pemba hawafuati uzazi wa mpango

TAKRIBANI asilimia 6.8 ya wakazi wa kisiwa cha Pemba mkoa wa Kusini ndio wanaotumia uzazi wa mpango, kiwango ambacho ni kidogo sana.

Waziri wa Maji, Nishati, Ardhi, Salama Aboud Talib alisema hayo wakati akizungumza katika siku ya idadi ya watu mjini Unguja.

Amewataka akinamama kuzingatia uzazi wa mpango kwa kushirikiana na wenza wao ili kuweza kuimarisha afya zao kuwa bora.

Amesema mikakati ya uzazi wa mpango ni sehemu ya malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika kuona wanawake wanakuwa na afya nzuri ambazo zitawawezesha kutekeleza majukumu yao ya kiuchumi na maendeleo.

''Uzazi wa mpango ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuwalinda wananchi wake kuwa na afya bora itakayowawezesha kuongeza uzalishaji mali na uchumi,'' amesema.

Naibu Waziri wa Afya, Harusi Said Suleiman amesema, utafiti umefanywa ambao umegundua kwamba asilimia 96 ya akinamama wanaojifungua majumbani, hutumia dawa za mitishamba kuweza kujifungua kwa haraka.

Amesema, matumizi ya dawa za mitishamba kwa ajili ya kupunguza maumivu hazikubaliki kwa sababu hazipo kitaalamu, zaidi zikiwa na madhara mengi kwa afya ya akinamama.

''Msimamo wa Wizara ya Afya upo wazi ni kuwataka akinamama kujifungulia hospitalini chini ya uangalizi wa madaktari bingwa,'' alisema.

Mapema Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), Jacqueline Mahon alisema matarajio makubwa ni kuona akinamama wanashiriki katika uzazi wa mpango, ambao utawapa nafasi kubwa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuchumi.

Aidha amesema, UNPFA ipo tayari kushirikiana na SMZ na kuona changamoto zote zinazowakabili wanawake, ambazo ni kikwazo katika maendeleo zinatatuliwa hatua kwa hatua. Ujumbe wa siku ya idadi ya watu ni 'Uzazi wa mpango ni utekelezaji wa haki za binaadamu’.

Rais John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi