loader
Picha

Tume kuchunguza wanafunzi kutozwa fedha wakichelewa

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud ameunda tume ya watu watano kuchunguza madai ya wanafunzi wa shule ya Mwembeladu kuchangishwa fedha, wakati wanapochelewa kufika shule, ikiwa ni sehemu ya adhabu.

Mahmoud amesema hayo wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya wanafunzi hao kutoa malalamiko yao mbele ya waandishi wa habari katika kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangaza la Zanzibar (ZBC).

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imefuta michango yote kutoka kwa wazazi katika sekta ya elimu kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wazazi gharama za elimu.

Alifahamisha kitendo cha walimu kuwachangisha wanafunzi, ikiwa ni sehemu ya adhabu hakikubaliki, kinakwenda kinyume na agizo la serikali ambalo limefuta michango.

''Nimeamua kutangaza tume ya watu watano ambayo itachunguza tuhuma za walimu wa shule ya Mwembeladu kuhusu vitendo vya kuwachangisha wanafunzi fedha ikiwa ni mbadala wa adhabu,'' amesema.

Alisema tume hiyo itaongozwa na Katibu tawala, Ofisa wa Jeshi la Polisi, Usalama pamoja na ofisa mmoja kutoka mamlaka ya kuchunguza rushwa na uhujumu wa uchumi.

Hakusema tume hiyo imepewa muda gani kukamilisha uchunguzi wake na kuwasilisha ripoti yake katika suala hilo.

Aidha Mahmoud amesema elimu ya msingi na maandalizi kwa sasa ipo katika mpango wa ugatuzi ambapo suala la michango ya wanafunzi limepigwa marufuku.

''Wapo baadhi ya walimu wanakaidi agizo la serikali na kuamua kuwachangisha wanafunzi fedha au wakati mwingine wanakataa kukagua kazi zao katika madaftari, hili halikubaliki tutalifanyia kazi,''alisema.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi