loader
Picha

Mkuza III tegemeo uchumi Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema Dira ya Maendeleo 2020 pamoja na Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupambana na Umasikini (Mkuza III), ndiyo tegemeo la kukuza uchumi ambao umejumuisha ushiriki wa sekta binafsi.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pemba Juma ameyasema jhayo wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi katika mkutano uliowakutanisha watendaji wa SMZ, wakiwemo makatibu wakuu na manaibu kuhusu majadiliano ya kiuchumi na maendeleo.

Pembe amesema, mpango wa dira ya maendeleo 2020 umehusisha sekta binafsi ambayo imepewa jukumu kubwa katika kukuza uchumi, huku serikali ikiyatangaza maeneo huru ya uchumi kwa ajili ya kutumika katika sekta ya uwekezaji.

Amesema, kazi kubwa inayofanywa na serikali kwa sasa ni kuyatangaza maeneo huru ya kiuchumi yaliyopo Fumba na Micheweni, na kuwataka wawekezaji, ikiwemo wazalendo kujitokeza kuwekeza katika miradi ya maendeleo, hasa ujenzi wa viwanda vya aina mbalimbali.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Iddi Makame amesema, matarajio makubwa ya mjadala huo ni kuibua changamoto zenye lengo la kujenga uchumi ambao utakuwa na tija kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Mwakilishi wa Taasisi ya Uongozi anayeshughulikia masuala ya mafunzo, Kadari Singo alisema majadiliano hayo yaliyowahusisha watendaji wakuu wa serikali ni kwa ajili ya kujenga hoja ambazo zitaibua katika kukuza na kuimarisha uchumi.

Rais John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi